1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO: Shinzo Abe abadili baraza lake la mawaziri

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVT

Waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, leo amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri na uongozi wa chama tawala katika juhudi zake za kujiimarisha huku umaarufu wake ukiendelea kushuka nchini humo.

Shinzo Abe amemteua Nobutaka Machimura kuwa waziri wa mashauri ya kigeni, wadhifa aliokuwa nao katika serikali ya waziri mkuu wa zamani wa Japan, Junichiro Koizumi. Aliyekuwa waziri wa sheria na mashauri ya kigeni, Masahiko Komura, ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi.

Katibu wa baraza la mawaziri la Japan amesema anaamini waziri mkuu Shinzo Abe amewateua viongozi wanaoweza kutekeleza wajibu wao, lakini akaonya kuwa hakuna njia ya mkato itakayomuwezesha waziri mkuu Shinzo Abe kupata uungwaji mkono kwa haraka katika baraza lake la mawaziri.