TOKYO: Marekani yatangaza Korea Kaskazini imekubali kurejea kwenye mashauriano ya pande sita. | Habari za Ulimwengu | DW | 20.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOKYO: Marekani yatangaza Korea Kaskazini imekubali kurejea kwenye mashauriano ya pande sita.

Mawaziri wa nje wa Jordan na Misri ziarani Jeruselem

Mawaziri wa nje wa Jordan na Misri ziarani Jeruselem

Mjumbe wa Marekani kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini, Christopher Hill, amesema serikali hiyo imekubali kurejea haraka iwezekanavyo kwenye mashauriano ya pande sita kuhusu mradi wake wa silaha za kinyuklia.

Christopher Hill alikuwa akizungumza baada ya mashauriano kati yake na mjumbe wa Japan mjini Tokyo, kituo chake cha pili cha ziara ya mataifa ya Eshia.

Mjumbe huyo wa Marekani alisema mashauriano ya hivi karibuni mjini Berlin yaliweka msingi mzuri wa mkutano wa pande sita utakaoandaliwa nchini China.

Baada ya mkutano wa Berlin, Korea Kaskazini ilisema ilikuwa imeafikiana kwa namna fulani na Marekani.

Mazungumzo ya pande sita yalirejewa mwezi Disemba mwaka uliopita baada ya kusitishwa kwa muda wa mwaka mmoja.

Korea Kaskazini ilitumia muda huo kufanya jaribio lake la kwanza la bomu la kinyuklia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com