TOKYO: Kimbunga Man Yi chavuma visiwani Okinawa | Habari za Ulimwengu | DW | 13.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TOKYO: Kimbunga Man Yi chavuma visiwani Okinawa

Kimbunga kikali kimevuma katika visiwa vya Okinawa,kusini mwa Japan.Zaidi ya watu 100,000 wamebakia bila ya umeme na idadi fulani ya nyumba zimesombwa na mvua kubwa zilizosababishwa na kimbunga Man-Yi.Vile vile zaidi ya watu 8,000 wameshauriwa kuhamia kwengineko.Kama safari 400 za ndege zimefutwa.Siku ya Jumamosi,kimbunga hicho kinatazamiwa kufika magharibi ya Japan kwenye kisiwa cha Kyushu,ambako tayari maelfu ya watu wamehamishwa sehemu zingine.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com