1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TIRANA:Rais Bush afanya ziara Albania

Rais Gorge W Bush wa Marekani amewasili nchini Albania katika ziara yake ya barani Ulaya .

Albania inatarijia kutoka kwa rais Bush kupata hakikisho la kuungwa mkono katika kujiunga na umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi NATO pamoja na kupatikana mwafaka katika suala la hatma ya jimbo la Kosovo.Ziara ya Bush imepokelewa kwa furaha na Waalbania wengi ambao wanasema itakuwa ya manufaa kwa nchi yao na hatma jimbo la Kosovo.

Marekani inaunga mkono kwa dhati mpango wa Umoja wa mataifa wa kutaka uhuru kwa jimbo la Kosovo mwaka huu hatua ambayo inapingwa vikali na Urussi ambaye ni mshirika wa Serbia.

Ulinzi mkali umewekwa katika barabara za mji wa Tirana ambako hakutarajiwi kufanyika maandamano ya kupinga ziara hiyo.

Baadae rais Bush anatarajiwa kukamilisha ziara yake nchini Bulgaria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com