TIBILIS:Rais wa Georgia azidi kuitupia lawama Uurusi | Habari za Ulimwengu | DW | 08.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TIBILIS:Rais wa Georgia azidi kuitupia lawama Uurusi

Rais Mikhail Saakashvili wa Georgia ameilaumu Urusi kwa kujaribu kuanzisha mtafaruku nchi mwake kufuatia ndege zake kuangusha mabomu hapo jana katika ardhi ya Georgia.

Rais Saakashvili aliyasema hayo karibu na eneo ambalo kombora moja lenye uzito wa tani moja lilidondoshwa na ndege za Urusi .

Maafisa wa Urusi wamekanusha taarifa hizo na kusema kuwa ni ndege za Georgia zenyewe zilizofyatua makombora hayo kwenye eneo lake ili kuchochea hali ya uhasama kati ya nchi hizo.

Georgia imesema kuwa mitambo yake ya kiulinzi imenasa picha zinazoonesha ndege za kirusi zikiingia katika anga ya Georgia na kuangusha makombora hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com