THE HAGUE: Taylor agoma tena kufika mahakamani
25 Juni 2007Matangazo
Aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor amesusia kesi yake iliyopangwa kusikilizwa tena leo mjini The Hague.
Wakili wake amesema kuwa bwana Taylor alimpigia simu na kumfahamisha kuwa hataenda mahakamani lakini hakuna sababu iliyotolewa.
Taylor anakabiliwa na madai juu ya kutenda uhalifu wa kivita hasa kutokana na kuwaunga mkono waasi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.