The Hague: Simic ahukumiwa miaka 15 jela. | Habari za Ulimwengu | DW | 28.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

The Hague: Simic ahukumiwa miaka 15 jela.

Korti ya rufaa ya mahakama ya kimataifa kuhusu Yugoslavia, imemhukumu mwanasiasa wa Bosnia Blagoje Simic kifungo cha miaka 15 jela,ikiwa ni miaka miwili kasoro ya ile hukumu ya hapo awali ya miaka 17 jela. Korti hiyo ililifuta shitaka moja wapo la uhalifu wa kivita, lakini ikaidhinisha kupatikana kwake na hatia kwamba Simic alisaidia kuangamizwa kwa raia wasio Warserbia katika mji wa Bosanski Samac , wakati wa vita vya Bosnia. Wanamgambo wa Kiserbia waliutwaa mji huo kaskazini mwa Bosnia Aprili 1992. Raia walikamatwa na kuzuiliwa katika hali ya kinyama ,waliteswa ikiwa ni pamoja na kun´golewa meno na wanawake kubakwa. Wakati huo daktari wa zamani Simic, alikua ni kiongozi wa ngazi ya juu mjini humo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com