THE HAGUE: Katibu Mkuu Ban ziarani Uholanzi
1 Februari 2007Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewasili Uholanzi ambako mbali na kukutana na Malkia Beatrix na waziri mkuu Jan Peter Balkenende,atatembelea pia Mahakama ya Uhalifu wa Kivita pamoja na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.Uholanzi ni kituo cha mwisho cha Ban katika ziara yake barani Ulaya na Afrika.