1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko kubwa la ardhi kisiwani Martinique

30 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CV7B

Tetemeko kubwa la ardhi limetokea katika kisiwa cha Ufaransa Martinique kwenye Bahari ya Karibea. Mwanamke mmoja mzee amefariki baada ya kupata mshtuko wa moyo na watu 6 wamejeruhiwa.Tetemeko hilo lenye nguvu ya 7.4 katika Kipimo cha Richter,limeteketeza idadi kubwa ya nyumba kisiwani Martinique na hata katika kisiwa cha jirani Barbados.Kama nyumba 16,000 kiswani Martinique hazina umeme.