1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV:Israel yapuuza ripoti kuhusu mpango mzima wa Iraq

7 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClk

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert amepuuzilia mbali baadhi ya mapendekezo yaliyochapishwa katika ripoti ya Tume ya Utafiti mahsusi kwa Iraq.Kwa upande wake kiongozi huyo anapinga hatua ya kufanya mazungumzo na Syria kama mshirika wa mpango mzima wa Mashariki ya kati.

Bwana Olmert anaeleza kuwa ripoti hiyo ilifanya kosa kuhusisha matatizo nchini Iraq na mzozo kati ya Waarabu na Israeli.Ripoti hiyo inapendekeza kuwa taifa la Israel lirejeshe milima ya Golan iliyoteka kutoka Syria katika vita vya siku sita mwaka 67 ili kujaribu kukata miguu juhudi za Syria za kuunga mkono wanamgambo wa Palestina.