TEL AVIV: Wanamgambo wa Kipalestina warusha kombora Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 26.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEL AVIV: Wanamgambo wa Kipalestina warusha kombora Israel

Licha ya kuwa na makubaliano ya kusitisha mapigano, wanamgambo wa Kipalestina tena wamerusha makombora dhidi ya Israel.Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Israel,makombora mawili yaliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza yameanguka katika mji wa Sderot.Kundi la Islamic Jihad la Wapalestina linasema,litakubali kuweka chini silaha,pale Israel itakapositisha harakati zake za kijeshi kwenye Ukingo wa Magharibi uliokaliwa. Kuambatana na makubaliano ya kuweka chini silaha, vikosi vya Israel vimeondoka kutoka Ukanda wa Gaza.Hata hivyo,rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas amemuahidi waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert kuwa makundi yote yenye silaha yatasitisha mashambulio yao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com