1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Waisraeli wanakumbuka mauaji ya Rabin

5 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvz

Zaidi ya Waisraeli 100,000 wamekusanyika mjini Tel Aviv kuadhimisha mwaka wa 11 tangu kuuawa kwa Yitzhak Rabin aliekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. Baadhi ya watu walibeba mabango yaliyotoa wito wa kuwa na amani na ustahmilivu.Mnamo mwaka 1994, Rabin na naibu waziri mkuu wa hivi sasa wa Israel,Shimon Perez na mwenyekiti wa chama cha PLO wakati huo,marehemu Yasser Arafat,walipewa tuzo la amani la Nobel.Rabin,aliuawa tarehe 5 Novemba mwaka 1995 na Myahudi mwenye siasa kali za kizalendo aliepinga sera za Rabin za kuwapa Wapalestina ardhi kwa ajili ya kupata amani.