1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Shimon Peres achaguliwa kuwa rais wa Israil

14 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrt

Mwanasiasa mkongwe Shimon Peres amechaguliwa kuwa rais wa Israil.

Shimon Peres ndiye aliyekuwa mgombea wa pekee baada ya wagombea wawili kujitoa kwenye duru ya pili ya uchaguzi huo uliofanywa bungeni.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 83 na ambaye ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, kwa sasa hivi ni naibu waziri mkuu wa serikali ya muungano inayoongozwa na Waziri Mkuu Ehud Olmert.

Shimon Peres atachukua mahali pa rais wa sasa Moshe Katsav ambaye yumo likizoni tangu mwezi Januari.

Moshe Katsav amekataa kung´atuka hata baada ya madai kutolewa dhidi yake kwamba aliwabughudhi kimapenzi wafanyikazi wa kike.