1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tel Aviv. Condoleezza Rice ziarani mashariki ya kati.

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7A6

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice yuko mjini Jerusalem kwa mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina. Ziara yake hiyo inakuja kabla ya mkutano wa kimataifa unaotayarishwa na Marekani , baadaye mwezi huu wenye lengo la kufufua hatua za kuleta amani kati ya Israel na Palestina.

Mkutano huo ni jaribio jingine kutayarisha waraka wa pamoja kati ya Israel na Palestina utakaoonyesha uwezekano wa suluhisho la mataifa mawili. Lakini hali ya wasi wasi inayoendelea baina ya Israel na Palestina pamoja na mgawanyiko mkubwa kati ya makundi ya Wapalestina una maana kuwa katika eneo la mashariki ya kati watu wanashaka na nia ya mkutano huo.

Wakati huo huo mamia kwa maelfu ya watu wamejikusanya mjini Tel Aviv katika kumbukumbu ya waziri mkuu wa Israel Yitzhak Rabin na mshindi wa nishani ya Nobel ya amani ambaye aliuwawa katika maandamano ya amani katika mji huo miaka 12 iliyopita. Alipigwa risasi na Myahudi mwenye imani kali kwa juhudi zake za kuleta amani na wapalestina.