1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Bunge la Israel litamchagua rais mpya mwezi ujao

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3c

Bunge la Israil, Knesset, litamchagua rais mpya tarehe kumi na tatu mwezi ujao.

Hatua hiyo imetokana na uamuzi wa jopo la ushauri la bunge hilo.

Rais wa sasa Moshe Katsav anatarajiwa kumaliza kipindi chake cha miaka saba tarehe kumi na tano mwezi Julai.

Moshe Katsav kwa sasa hatekelezi shughuli zake za urais kutokana na madai kwamba aliwabughudhi kijinsia na kuwabaka wafanyi kazi kadha wa kike.