Tel Aviv: Ban Ki-moon ziarani Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 25.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Tel Aviv: Ban Ki-moon ziarani Israel

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon yuko nchini Israel, ziara yake ya kwanza nchini humo tangu ashike wadhifa huo miezi miwili iliopita. Bw Ban alikutana na Waziri wa ulinzi wa Israel Amir Peretz mara tu baada ya kuwasili mjini Tel Aviv na anapanga pia kuonana na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas. Lakini amesema hatokutana na Waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniya kutoka chama cha Hamas, ambacho kinaendelea kuyakataa masharti ya kukiataka kilaani matumizi ya nguvu na kitambue haki ya kuishi dola ya Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com