1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN.Watu 11 wameuwawa katika shambulio la bomu

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSB

Takriban watu 11 wameuwawa baada ya basi linalomilikiwa na walinzi wa mapinduzi kushambuliwa kwa bomu.

Mji wa Zahedan ulio karibu na mpaka wa Pakistan na Afghanistan kusini mashariki mwa Iran unakabiliwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya maafisa wa usalama na makundi yanayodhibiti biashara ya madawa ya kulevya.

Wakati huo huo mshauri wa kiongozi wa kidini wa Iran Ayatollah Ali khamenei amedokeza kuwa huenda Tehran ikazingatia juu ya kusimamisha mpango wake wa atomiki.