TEHRAN:Rais Bush aalikwa Iran akahutubie chuo kikuu | Habari za Ulimwengu | DW | 02.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN:Rais Bush aalikwa Iran akahutubie chuo kikuu

Chuo Kikuu cha Ferdowsi nchini Iran kimetoa mwaliko kwa Rais George Bush wa Marekani kutoa mhadhara chuoni hapo, ikiwa ni wiki moja baada ya Rais Mahmoud Ahmednejad wa Iran kupata mapokezi mabaya kwenye chuo kikuu nchini Marekani.

Mkuu wa chuo hicho kilichoko katika mji wa Mashhad amesema kuwa Rais Bush anaalikwa ili kujibu maswali ya wanafunzi na wahadhiri juu ya haki za binadamu na ugaidi.

Kabla ya hotuba yake katika chuo kikuu cha Columbia mjini New York, Rais Ahmednejad alitambulishwa na Rais wa chuo hicho Lee Bollingera kama dikteta katili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com