TEHRAN: Watu watatu wanyongwa kwa kuhusika katika mashambulio | Habari za Ulimwengu | DW | 14.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN: Watu watatu wanyongwa kwa kuhusika katika mashambulio

Iran imewanyonga watu watatu hii leo kwa kuhusika kwenye mashambulio ya mabomu mjini Ahvaz kusini magharibi mwa nchi hiyo mnamo mwaka wa 2005.

Wanaume hao walionyongwa katika gereza la Ahvaz ni wa mwisho miongoni mwa kundi la watu 10 walionyongwa katika miezi ya hivi karibuni baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mashambulio ya mabomu na kuvuruga usalama wa taifa.

Hapo awali watu 18 waliuwawa katika shambulio la bomu dhidi ya basi kusini mashariki mwa Iran. Basi hilo lilikuwa limewabeba walinzi wa mapinduzi, lakini haikubainika wazi ikiwa miongoni mwa waliouwawa walikuwa ni walinzi.

Kwa mujibu wa walioshuhudia shambulio hilo, wanamgambo waliweka motokaa iliyokuwa na bomu katika barabara ilikopitia basi hiyo na kuiripua wakati basi ilipokuwa ikipita.

Shambulio hilo limefanywa mjini Zahedan karibu na mpaka wa Pakistan na Afghanistan, eneo ambalo linakabiliwa na mapigano makali baina ya maofisa wa usalama na makundi yenye silaha yanayohusika katika biashara ya madawa ya kulevya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com