1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Waandamana kupinga mgawo wa petroli

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnn

Watu wenye hasira wameandamana katika miji mbalimbali nchini Iran kupinga hatua ya serikali kutangaza mgawo wa petroli.

Televisheni ya serikali ya Iran ilitangaza kuwa vituo kadhaa vya mafuta vilishambuliwa na kwamba watu wamekamatwa kuhusiana na vurugu hizo.

Hatua hiyo ni katika juhudi za serikali kukabiliana na vikwazo vya Umoja wa Mataifa juu ya mpango wake wa nuklia.

Iran ni nchi ya pili duniani kwa kuzalisha kwa wingi mafuta yasiyosafishwa , lakini kutokana na uwezo mdogo wa kusafisha inaagiza zaidi ya asilimia 40 ya mafuta kutoka nje.