TEHRAN : Mwandishi Mmarekani - Muirani aachiliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 06.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Mwandishi Mmarekani - Muirani aachiliwa

Mwandishi habari Mmarekani wa asili ya Iran amepewa ruhusa ya kuondoka nchini Iran baada ya kushikiliwa na serikali kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.

Parinaz Azimi alikwenda Iran mwezi wa Januari kumtembelea mama yake alie mgonjwa lakini paspoti yake ilitaifishwa na maafisa wa serikali ya Iran ambayo ilimshtaki kwa makosa yanayohusiana na usalama.Azimi anafanya kazi na idhaa ya lugha ya Kiajemi nchini Marekani ya Radio Free Europe ambayo inagharamiwa na Marekani.

Bado haijulikani nini kilichopelekea kuachiliwa kwake mapema wiki hii mwanataaluma Mmarekani mwenye asili ya Iran aliruhusiwa kuondoka nchini Iran baada ya kusota gerezani kwa miezi kadhaa.

Wamarekani wengine wawili bado wako mahabusu nchini Iran.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com