TEHRAN : Iran iko tayari kwa lolote kutoka Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 25.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN : Iran iko tayari kwa lolote kutoka Marekani

Iran imesema iko tayari kwa lolote lile llitakalofanywa na Marekani kuzuwiya mpango wake wa nuklea.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Manouchehr Mottaki amewaambia waandishi wa habari kwamba wako tayari kwa hatua yoyote ile itakayochukuliwa na Marekani na kwamba hawaioni Marekani kuwa iko kwenye nafasi ya kuwatwika mgogoro mwengine walipa kodi wake kwa kuanzisha vita vyengine Mashariki ya Kati.

Kauli yake hiyo inakuja baada ya Makamo wa Rais wa Marekani Dick Cheney akiwa ziarani nchini Australia kutowa onyo kali dhidi ya Iran kwa kusema kwamba wakati wakipendelea kuendelea kutumia diplomasia kuutatuwa mzozo huo hatua zozote zile zinaweza kuchukuliwa kuizuwiya Iran kutengeneza silaha za nuklea.

Cheney amesema wanaamini litakuwa kosa kubwa kabisa iwapo taifa kama Iran litaachiliwa kuwa na nguvu za silaha za nuklea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com