TEHERAN: Msomi Esfandiari amezuiliwa nchini Iran
15 Mei 2007Matangazo
Msomi wa Kimarekani mwenye asili ya Kiirani,Haleh Esfandiari,amezuiliwa katika jela ya Evin mjini Teheran.Msemaji wa mahakama,Alireza Jamshidi alipozungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Teheran alisema,msomi huyo wa kike,hivi sasa amezuiliwa na idara ya upelelezi ya Iran katika jela ya Envin kwa mashtaka ya kwenda kinyume na usalama wa taifa na kwamba uchunguzi unaendelea kufanywa.