TEHERAN :Iran yakataa wazo la kusimamisha mpango wa kurutubisha madini ya uranium | Habari za Ulimwengu | DW | 09.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHERAN :Iran yakataa wazo la kusimamisha mpango wa kurutubisha madini ya uranium

Iran imekataa wazo la kusimamisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium baada ya mataifa makubwa sita kukubaliana juu ya kujadili uwezekano wa kuiwekea nchi hiyo vikwazo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran ameeleza kuwa nchi yake haikubaliani na wazo hilo na kwamba tishio juu ya kuiwekea vikwazo nchi yake halitafaa kitu.

Wawakilishi wa nchi tano wanachama wa kudumu kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani walikutana mjini London hivi karibuni kuzungumzia juu ya msimamo wa Iran wa kukataa kusimamisha shughuli za kurutubisha madini ya Uranium.

Nchi hizo zinahofia kuwa Iran inakusudia kuunda silaha za nyuklia lakini Iran imesisitiza kuwa mpango wake unalenga shabaha za amani tu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com