1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tchad yailaumu Sudan kuhujumu vijiji vyake vinne

28 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCyO

Djamena/New York

Serikali ya Tchad imelituhumu jeshi la anga la Sudan kuhujumu kwa mabomu vijiji vinne vya mpakani huko Bahai,Tine,Karyari na Bamina.Serikali ya Tchad imeutaka umoja wa Afrika,jumuia ya nchi za Sahel na sahara-CEN Sad na Umoja wa mataifa ulaani mashambulio hayo na kuilazimisha Sudan isitishe haraka hujuma zake.Msemaji wa seerikali ya Tchad Hourmadji Moussa Doumgor amesema vikosi vya usalama vya Tchad vimeamrishwa kuchukua hatua zinazostahiki kulinda usalama wa taifa.Msemaji huyo wa serikali hakusema lakini kama kuna waliouwawa kufuatia masha mbulio hayo ya jeshi la wanaanga la Sudan.Wakati huo huo mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa Jean Marie Guehenno ameliomba baraza la usalama lifikirie uwezekano wa kutuma tume ya ukaguzi au wanajeshi wa kulinda amani nchini Tchad kutokana na kuzidi mzozo katika jimbo la Darfour.