1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tayari kuua kwa euro nane

4 Februari 2011

Misri Cairo ingali tete. Wapinzani na wafuasi wa serikali wanapambana na wanarushiana mawe.Hali ya mambo katika mji mkuu wa Waandishi wa habari wanaripoti juu ya ukatili wanaoshuhudia.

https://p.dw.com/p/Qy9x
A wounded anti-government protestor reacts as he is being treated in Tahrir Square, Cairo, Egypt, Friday, Feb. 4, 2011. The Egyptian military guarded thousands of protesters pouring into Cairo's main square on Friday in an attempt to drive out President Hosni Mubarak after a week and half of pro-democracy demonstrations. (AP Photo/Emilio Morenatti)
Wapinzani wa serikali walishambuliwa uwanja wa TahrirPicha: AP

Kwa mujibu wa kijana mmoja aliyeshiriki katika maandamano hayo kwenye uwanja wa al-Tahrir mjini Cairo, wafuasi wa Rais Hosni Mubarak walikuwa tayari kuuwa kwa malipo ya kiasi cha Euro nane. Kijana Muhammad Fathi ni mkalimani mwenye umri wa miaka 22 na yeye ni mmojawapo wa waandamanaji waliokusanyika kwenye uwanja wa al-Tahrir katikati ya mji mkuu Cairo na amejaribu kueleza yale aliyoshuhudia.

"Kilichotokea ni mauaji ya mpangilio. Tulizingirwa kuanzia saa nane za mchana hadi saa kumi na mbili asubuhi. Tulishambuliwa na maelfu ya watu - yaani walioajiriwa kushambulia, wahalifu walioachiliwa kutoka jela, polisi na askari wa usalama waliokuwa katika mavazi ya kiraia. Hata maafisa wa polisi walikuwemo miongoni mwao."

Pro-government demonstrators, bottom, clash with anti-government demonstrators, top, in Tahrir Square, the center of anti-government demonstrations, in Cairo, Egypt, early Thursday, Feb. 3, 2011. Thousands of supporters and opponents of Egyptian President Hosni Mubarak battled in Cairo's main square all day Wednesday, raining stones, bottles and firebombs on each other in scenes of uncontrolled violence as soldiers stood by without intervening. Government backers galloped in on horses and camels, only to be dragged to the ground and beaten bloody. (AP Photo/Lefteris Pitarakis)
Wafuasi wa Mubarak na wapinzani wake waliopambana vikaliPicha: AP

Kuna ushahidi mbali mbali kuhusu tuhuma hizo. Wagombea demokrasia waliwakamata washambuliaji hao na waliwakabidhi wanajeshi. Washambuliaji hao walikuwa na vitambulisho vyao vya askari. Wengi wao walikiri kuwa walilipwa kuwashambulia waandamanaji yaani Euro nane hadi themanini kwa kitendo cha kuua. Hadi hiyo jana washambuliaji hao walionekana ukingoni mwa uwanja wa Tahrir, wakipandishwa katika mabasi na wakipewa mabomu ya petroli kabla ya kupelekwa kwenye uwanja huo mjini Cairo.

Tangu jana hata waandishi wa habari wa kigeni wanazuiliwa kufanya kazi zao, wanapigwa na wanakamatwa. Kwa upande mwingine, vichwa vya habari katika magazeti rasmi nchini Misri vinasema "Misri imeibuka imara zaidi kufuatia mgogoro huo" au "Hili ni shambulio hatari kabisa la kigeni dhidi ya Misri." Na wagombea demokrasia wanaelezwa kama ni kundi la wafanya ghasia.

Wakati huo huo, Makamu wa rais wa Misri, Omar Suleiman, ambae siku chache zilizopita alizungumzia kufanya majadiliano, sasa ametoa masharti: Atazungumza na vyama vya upinzani ikiwa tu maandamano hayo yatamalizika.

Mwandishi: Saoub,Esther/ZPR
Tafsiri:P.Martin
Mpitiaji: Miraji Othman