Tanzania yazindua Mgodi rasmi wa madini | Masuala ya Jamii | DW | 21.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Tanzania yazindua Mgodi rasmi wa madini

Serikali ya Tanzania imezindua rasmi mgodi wake wa kwanza utakaowaajiri wafanyakazi wazawa tu kuanzia ngazi za uongozi hadi chini.

Hatua hiyo imechukuliwa na serikali kama juhudi za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa watanzania.Aidha waziri wa nishati na madini nchini humo Sospeter Muhongo amesema mgodi huo wa dhahabu wa Biharamulo utafuatiwa na mingine kadhaa itakayotowa pia nafasi za ajira kwa wazawa ingawa amesisitiza Tanzania haina nia ya kuwafukuza wageni wanaosimamia migodi mingine ya nchi hiyo . Saumu Mwasimba amezungumza nae mchana huu na kutupa maelezo kamili kuhusu mgodi huo na hatua hiyo ya serikali. Kuskiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Saumu Yusuf

Mhariri: Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada