Tanzania yasaini mkataba wa reli wa dola bilioni 2 na China
21 Desemba 2022Matangazo
Reli hiyo yenye urefu wa kilometa 2,561 itaunganisha bandari ya Dar es Salaam hadi Mwanza na hatimaye kuelekea Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeshuhudia utiaji saini huo, amesema nchi hiyo inapaswa kukopa kwa ajili ya miundombinu muhimu na miradi mingine ya maendeleo endelevu huku akipuuza ukosoaji kwamba nchi inakabiliwa na mzigo wa madeni.
Bi.Samia ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha mwisho wa reli ya kisasa SGR chenye urefu wa kilomita 506 kutoka Tabora hadi Kigoma utakamilika mwaka 2026, miaka tisa tangu ujenzi wake ulipoanza.