Tanzania-Stars kwenda Ghana 2008 ? | Michezo | DW | 18.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Tanzania-Stars kwenda Ghana 2008 ?

Simba wa nyika Kamerun,Morocco na Angola zimeshatia tiketi zao kwenda Ghana 2008 kwa finali za Kombe la Afrika. Tanzania-Taifa Stars hatima yao itategemea ushindi nyumbani dhidi ya Msumbiji.

Real Madrid wameipiku dakika za mwisho FC Barcelona jana kwa kuikomea Real Mallorca mabao 3:1.Ilikua Marlloca lakini, iliotangulia kutia bao,na zikisalia dakika 17 tu ikionekana Mallorca imeivalisha taji Barcelona, Real Madrid ilimtoa David Beckham na kumuita uwanjani Reyes alieufumania mlango wa Real Marlloca na kusawazisha bao 1:1.Kwanza ilikua Fernando Varela aliewanyamazisha mashabiki 76.000 wa Real Madrid uwanjani alipotia bao la kwanza la Mallorca.

Wakati David Beckham anaiachamkono Real akiwa na zawadi maalumu ya ubingwa, FC Barcelona pamoja na mastadi wake akina Ronaldinho na Samuel Eto’o imeondoka msimu huu mikono mitupu.

Katika Bundesliga –iliomaliza msimu wake kwa kuitawaza Stuttgart mabingwa wapya, rais wa Bayern Munich Karlheinz Rummenigge alisisitiza jana kwamba Munich haitaridhia kuchezeshwa kamari na Bremen kuhusu kumuajiri mshambulizi wa Werder Bremen na wa timu ya taifa Miroslav Klose.Klose alikwishatangaza kwamba atajiunga na Munich msimu wa 2008,lakini Bayern Munich inamtaka tayari Klose msimu huu utakapoanza hapo August.Bremen haipingi lakini inataka kumbadilisha-Klose kwa Lukas Podolski.Bayern Munich yaonesha haiko tayari kucheza kamari hiyo-asema Karlheinz Rummengige.

Rais wa shirikisho la dimba la Ujerumani DFB Dr.Theo Zwanziger amesema kujiunga na Bayern Munich kwa mastadi 2 wa kombe lililopita la dunia-Frank Ribery wa Ufaransa na Lucatoni wa mabingwa wa dunia-Itali, ni kuinawirisha Bundesliga.Munich imetumia Euro milioni 36 kuwanunua mastadi hao 2.

Katika kinyan’ganyiro cha Kombe la Afrika la mataifa, Simba wa nyika-Kamerun,Morocco na Pia Angola zimeshakata tiketi zao za kwenda Ghana 2008 kwa finali za kombe hilo.

Kwa ushindi wa Taifa Stars-Tanzania wa bao 1:0 dhidi ya Burkina Faso huko Ouagadogou na kutoka suluhu 0:0 Senegal na Msumibiji,matumaini ya Taifa Stars kwenda Ghana hyakuwahi kunawiri zaidi. Huko Tanzania dimba lilichezwa leo hadi bungeni. Taifa Stars walipokelewa Bungeni mjini dodoma na kama zawadi ya ushindi wao wameahidiwa wachezaji na kocha wa kutoka Brazil kitita cha hadi TZsh.Milioni 100.Tanzania itacheza na Msumbiji hapo Septemba kuamua ni wao au Senegal watakwenda Accra.

Timu zote mbili zina pointi 8.Keenya imeapigwa kumbo nje ya mashindano baada ya kulazwa bao 1:0 na Eritrea mjini Asmara.

Riadha:wakati Kenya, imechagua wanariadha wake watakoiwakilisha mwezi ujao katika michezo ya bara la Afrika huko Algiers (All-Africa Games),

wakenya weengine wametamba katika mbio za kimataifa za km 10 mjini Jakarta,Indonesia jana.John Cheruiyot Korir alishinda upande wa wanaume wakati Rita Sitienei Jeptoo upande wa wanawake.Korir alifuatwa nafasi ya pili na ya tatu na wakenya wengine-Johnstone Chepkowny na Robert Kipkorir.Washindi kila upande, waliondoka Jakarta na kitita cha dala 11.000.Wale wapili walichotqa dala 6000 kila mmoja.