1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Vyombo vya habari

Tanzania: Nipashe Jumapili lajifungia lenyewe

16 Januari 2018

Kampuni ya habari ya IPP Media imefungia gazeti lake la Nipashe Jumapili kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuandika kichwa kisemacho: "JPM akerwa wanaomtaka adumu urais kama Kagame."

https://p.dw.com/p/2qvi3
Gazeti la Nipashe Jumapili
Picha: DW/E.Boniphace

Ni katika kile kilichosemekana kama kuenzi uwajibikaji baada ya kuchapisha habari iliyohusu rais Magufuli kutaka watu wasiendeleze mjadala kuhusu ukomo wa urais na kuufananisha na utawala wa rais Paul Kagame wa Rwanda ni jambo linaloendelea kuzua gumzo nchini Tanzania. 

Gazeti la Nipashe Jumapili limejifungia kwa miezi mitatu pamoja na kumuomba radhi Rais Mafufuli na Rais Kagame. Lakini baadhi ya wadadisi wanahisi hatua hiyo ya gazeti la Nipashe haikustahili. Kwa mengi zaidi DW imezungumza na mwandishi mkongwe katika tasnia hii ya uandishi habari Salim Salim aliyeko nchini Tanzania na kwanza anatoa maoni yake juu ya hatua hiyo.