1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Maandamano ya chama cha Chadema mjini Arusha

5 Januari 2011

<p>Chama cha upinzani cha Chadema huko Tanzania kilifanya maandamano na mkutano wa hadhara leo mjini Arusha, kaskazini mwa Tanzania, na matokeo ni kutokea mapambano baina ya waandamanaji na polisi.

https://p.dw.com/p/ztxW
Inasemekana kuna watu waliojeruhiwa na pia maafisa wa vyeo vya juu wa chama hicho kutiwa mbaroni.

Chadema kilitangaza tangu kumalizika uchaguzi mkuu wa Oktoba  mwaka jana nchini Tanzania kwamba kitafanya  maandamano nchini kote kuibinya serikali ifanye  marekebisho ambayo chama hicho  kinasema ni muhimu yafanyike nchini humo.

Othman Miraji alizungumza na Dr. Wilbrod Slaa, mtetezi wa chama cha Chadema katika uchaguzi uliopita wa urais na aliyeshiriki leo katika maandamano ya Chadema huko Arusha...

Mhariri: Othman Miraji

Mpitiaji : Josephat Charo