1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yashutumiwa kuwateka nyara raia wa Taiwan

Mjahida 12 Aprili 2016

Taiwan imesema kuna njama ya kuwapeleka China raia wake 37 waliyoko kizuizini nchini Kenya, hii n i baada ya Taiwani kudai China imewateka nyara kundi la waitaiwan wapatao wanane kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki.

https://p.dw.com/p/1ITjI
Taiwan Tsai Ing-wen und Ma Ying-jeou in Taipeh
Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen akiwa pamoja na rais anayeondoka wa Taiwan Ma Ying-jeouPicha: picture alliance/AP Photo/Sun Chung-ta

"Asubuhi ya leo tulifahamishwa kuwa Kenya inaweza kuwasafirisha raia wetu China, wenzetu walikwenda moja kwa moja hadi katika jela za kenya lakini wakakabiliwa na vikwazo," alisema Chen Chun-shen, Mkuu wa masuala ya Magharibi mwa Asia na Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya Taiwan alipokuwa anazungumza na waandishi habari mjini Taipei.

Shen amesema China imetoa shinikizo kwa Kenya ili raia hao wasafirishwe nchini humo huku akisema kuwa kati ya wataiwan hao wanane ambao tayari wamepelekwa Beijing na serikali ya Kenya mmoja wao anasemekana kuwa na paspoti ya Marekani.

Hata hivyo serikali ya China bado haijathibitisha kuwapokea raia hao wa Taiwan na Taipei bado inatafuta majibu.

China inaiona Taiwan kama sehemu ya eneo lake linalosubiri kuunganishwa, hata kwa kutumia nguvu kama hilo litahitajika, licha ya kwamba Taiwan yenyewe ilijiondoa tangu mwaka wa 1949 baada ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na serikali hiyo ya kikomunisti.

Li Keqiang
Waziri Mkuu wa China Li KeqiangPicha: Reuters/How Hwee Young

Taiwan yasema Kenya ilitumia nguvu kwa raia wake

Kulingana na wizara ya mambo ya kigeni nchini Kenya, Katika kundi hilo la watu 37, 15 waliondolewa mashtaka na Korti moja nchini humo kwa madai ya kuhusika katika uhalifu wa mitandao.

Wengine 22 waliyobakia ambao kwa sasa wapo ndani ya ndege ya China wakisubiri kuondoka, hawakufikishwa mahakamani kwa madai hayo hayo ya uhalifu wa mitandao.

Kwa upande wake Mwenda Njoka msemaji wa wizara ya ndani ya Kenya amesema watu hao walikuwa nchini Kenya kinyume cha sheria na walikuwa wanarejeshwa kule walikotoka.

Taiwan Republik China Flagge
Bendera ya TaiwanPicha: picture-alliance/dpa/J. Favre

"Walikuja kutoka China na tumewarejesha huko huko walikotoka, kwa kawaida unapoingia katika nchi yoyote kinyume cha sheria unarejeshwa kule ulikotokea." Alisema Njoka.

Wakati huo huo Taiwan imeishitumu Kenya kwa kutumia nguvu kupita kiasi kuwalazimisha raia wake kupelekwa china msemaji wa wizara ya nje Chen shen anasema

Aidha polisi ya kenya ilipoulizwa kuhusu madai hayo ilisema nchi hiyo inawajibu wa kuwarejesha watu walioko huko kinyume cha sheria katika maeneo walikotoka. Takriban nchi 22 zinaitambua Taiwan kama Jamhuri ya China ikiwemo Kenya iliyo na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na China na inayotambua China moja - hii ikiwa ndiyo sera ya viongozi chama tawala ya kikomunisti.

Mwandishi Amina Abubakar/AFP/Reuters

Mhariri:Iddi Ssessanga