1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TAIPEI : Tetemeko laangusha nyumba kadhaa Taiwan

Mtetemeko mkubwa wa ardhi na mitetemeko midogo iliyofuatia tetemeko hilo kuu imepiga mwambao wa kusini mwa Taiwan na kusababisha majengo kadhaa kuanguka,kuuwa watu wawili na kujeruhi wengine kadhaa.

Tetemeko la kwanza lilikuwa na kiwango cha 7 cha kipimo cha richter.Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Japani ilitowa tahadhari ya tetemeko la Tsunami kwa Taiwan ya kusini na Ufilipino lakini masaa mawili baadae iliondowa onyo hilo.

Tetemeko hilo linakuja miaka miwili katika siku iliyotokea gharika la Tsnunami kwenye Bahari ya Hindi hapo mwaka 2004 ambalo lilipelekea kuuwawa kwa watu 230,000 kwenye mataifa kadhaa ya Asia.

Kumbukumbu ya kuwakumbuka wahanga ilifanyika hapo jana kwenye eneo lote la Asia lililoathirika na janga hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com