Syria yaendelea kutumia nguvu kukandamiza upinzani
21 Desemba 2011Matangazo
Kituo cha wanaharakati wa haki za binadamu wa Syria mjini London, kimeripoti kuwa wanajeshi 100 walioasi, walizingirwa na waliuawa au walijeruhiwa wilayani Idlib. Siku ya Jumatatu pia wanajeshi 70 walioasi waliuawa katika wilaya hiyo iliyo karibu na mpaka wa Uturuki. Wanaharakati wanasema, hapo jana vile vile raia 33 waliuawa huko Idlib na Homs.
Umoja wa Nchi za Kiarabu umesema, tume ya wajumbe wake kesho inakwenda Syria. Katika makubaliano yaliyopatikana siku ya Jumatatu kati ya umoja huo na Syria, serikali ya Rais Bashar al-Assad imekubali kuacha kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji, kuwaruhusu waangalizi nchini humo na kuyaondoa majeshi yake kutoka maeneo yaliyo ngome za upinzani.