Super Tuesday
6 Februari 2008Matangazo
Takriban kura zilizopigwa jumanne ya jana "Super Tuesday" kutoka majimbo yote 24, zimeshahesabiwa -hata hivyo hakuna yeyote kati ya wagombea wawili wa chama cha Democratic aliyeibuka na ushindi bayana:Hilary Clinton na Barack Obama bado wanashindana-idadi ya kura zao takriban zinalingana.Hilary Clinton ameibuka na ushindi katika majimbo makubwa mfano Kalifornia,New-Jersey na New-York.Kwa upande wake Barack Obama ameshinda kama ilivyotarajiwa katika majimbo ya kusini wanakoishi wamarekani wengi weusi.Amejinyakulia ushindi katika majimbo 12 kati ya 21.Kisicho bayana hadi wakati huu,na hali hii inatokana na utaratibu mgumu wa upigaji kura wa chama cha Democratic,ni nani kati ya wagombea hao wawili aliyejikingia kura nyingi zaidi za wajumbe.
Hali bayana zaidi imejitokeza upande wa chama cha Republican:John McCain anaendelea kuongoza.Ingawa Mitt Romney na Mike Huckabee wameshinda katika jumla ya majimbo 11,lakini wako nyuma,mtu akitilia maanani idadi ya kura za wajumbe walizojikingia.McCain ameshinda zaidi Karlifonia na New-York -kwa namna hiyo mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 71 amejikingia sauti za wajumbe wote wa majimbo hayo makubwa.
Ni dhahiri kwa hivyo kwamba jana usiku aliyeshangirwa kua mshindi ni McCain.
"Leo hii tunaweza kudhibitisha,kwamba katika chama cha Republican ,sisi ndio tunao ongoza."
Hilary Clinton na Barack Obama nao pia wameshangiriwa na wafuasi wao.
Shangwe na furaha zilihanikiza kwa namna ambayo hapo awali Hilary Clinton alionekana kutopata nafasi ya kuhutubia.Lakini baadae Senetor huyo wa New York alipata fursa ya kuwaambia wafuasi wake kile ambacho walitaka kukisikia:
"Mko tayari kumchagua rais atakaezifikisha ikulu ya Marekani ,sauti zenu,maadili yenu na ndoto zenu".
Matumaini kama hayo yametolewa pia na Barack Obama katika jimbo lake la Chicago-ingawa hakufikiria kama angeshindwa katika jimbo muhimu la Karlifonia.Obama anasema:
"Kuna kitu ambacho ni muhimu zaidi katika siku hii ya leo ya February,kuliko matokeo ya mwisho:tunatambua wakati wetu umewadia."
Wote wawili Hilary Clinton na Barack Obama wametambua mnamo siku hii ya Super Tuesday-hakuna aliyeibuka na ushindi, upande wa chama cha Democratic-kampeni ya uchaguzi inaendelea.Jumamosi ijayo katika majimbo ya Nebraska na Washington na wiki ijayo katika jimbo la Maryland.
►
LINK: http://www.dw-world.de/dw/article/0,,3110879,00.html
Matangazo