1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Sudan yaregeza kamba

Umoja wa mataifa kushirikiana na Umoja wa Afrika huko Darfour

Ban Ki Moon ,Alpha Omar Konarena Salim Ahmed Salim katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa

Ban Ki Moon ,Alpha Omar Konarena Salim Ahmed Salim katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa

Viongozi wa Sudan wamefungua njia ya kutumwa tume ya pamoja ya kulimnda amani huko Darfour kwa kukubali helikopta za kijeshi za umoja wa mataifa ziimarishe nguvu za vikosi vya kulinda amani vya umoja wa Afrika.

Mpango wa Umoja wa mataifa unazungumzia juu ya kutumwa wanajeshi elfu tatu wa kulinda amani, na vifaa vya kijeshi kuwasaidia wanajeshi elfu sabaa za Umoja wa Afrika ambao tayari wanakutikana Darfour.

Khartoum lakini bado haijatoa ridhaa kama idadi ya wanajeshi izidishwe na kufikia 20 elfu.

Wanadiplomasia wa nchi za magharibi wanaamini aina ya ushirikiano utakaochipuka kati ya serikali ya mjini Khartoum na Umoja wa mataifa na hali namna itakavyokua katika jimbo la Darfour ndio mambo yatakayoamua kama ridhaa ya Khartoum itasaidia au la kuondolewa vikwazo ambavyo Washington na London wamedhamiria kuiwekea Sudan.

Lakini muakilishi wa Marekani Alejandro Wolff ameshasema hakuna uamuzi wowote bado uliopitishwa na kwamba serikali ya rais George W. Bush inasuburi arejee nyumbani kutoka Sudan naibu waziri wa mambo ya nchi za nje John Negroponte.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uengereza Margareth Beckett anasema:

“Tunaona kuna maendeleo kidogo na tunayakaribisha,lakini tunahitaji kuona maendeleo zaidi.”

“Ni ishara njema” amesema kwa upande wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon, aliyendelea kusema kwamba”Umoja wa Afrika na yeye binafsi wana azma ya kuwajibika haraka iwezekanavyo.” Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon alisema hayo mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa akiwa pamoja na mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Alpha Omar Konare.

Balozi wa Ufaransa katika umoja wa mataifa Jean Marc de la Sablière amesema „waanabidi waharakishe kutia njiani yaliyoafikiwa na kuzidisha majadiliano ya kuundwa kikosi cha mchanganyiko.

Balozi wa Ufaransa katika umoja wa mataifa amesema ufumbuzi wa kisiasa ndio njia pekee ya kuutatua mzozo wa Darouf.Jean Marc de la Sablière ameongfeza kusema baraza la usalama limezungumzia madhara ya hali katika jimbo la Darfour kwa eneo zima na hasa mashariki ya Tchad.

Nae kiongozi wa shughuli za kulinda amani za umoja wa mataifa Jean Marie Guéhenno amewaambia waandishi habari wanajeshi elfu tatu wa kulinda amani,helikopta na misaada mengineyo ya kimbinu ni mwanzo tuu wa kikosi kikubwa zaidi kinachohitajika Darfour.

Mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika ASlpha Omar Konare amesema wana vikosi viwili vya wanajeshi ambao wako tayari kwenda Darfour kutayarisha uwanja kabla ya kuwasili wanajeshi wa Umoja wa mataifa.Ameongeza kusema hata hivyo panahitajika fedha kuwahudumia wanajeshi hao wa Umoja wa Afrika.

 • Tarehe 17.04.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CB4g
 • Tarehe 17.04.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CB4g

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com