Sudan ya Kusini yasheherekea uhuru wake
9 Julai 2011Matangazo
Leo taifa jipya la Sudan ya Kusini limezaliwa baada ya vita vya miaka mingi kutaka sehemu hiyo ijitenge na Sudan. Sherehe na nderemo zimehanikiza katika mji mkuu wa Juba ambapo Salva Kiir ameapishwa kuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo. Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kukabiliana na mashtaka dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki huko Dafur.
Nimeungana sasa na mwandishi wetu wa Deutsche Welle huko Juba, Leylah Ndinda....Hebu tuelezee Leylah vipi siku ya leo ya kihistoria inavoadhimishwa