Sudan Kusini taifa jipya kabisa duniani
9 Julai 2011Matangazo
Kengele za kanisani zililia saa sita usiku, kuashiria siku hiyo ya kihistoria huku midundo ya ngoma ikilikaribisha taifa la 54 barani Afrika. Kuwepo kwa taifa hilo jipya, kutatangazwa rasmi leo asubuhi mjini Juba, katika sherehe zitakazofanywa, pale Rais Salva Kiir atakapoapishwa rais wa kwanza wa taifa hilo jipya.
Wakaazi katika mji mkuu Juba, walianza kusherehekea uhuru wa taifa lao tangu Ijumaa jioni kwa muziki na kupiga honi za magari mitaani.
Wiki ijayo Sudan Kusini inatazamiwa kupokewa kama nchi mwanachama wa 193 katika Umoja wa Mataifa.