Stuttgasrt yaizaba Munich 3:1 | Michezo | DW | 12.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Stuttgasrt yaizaba Munich 3:1

Mabingwa wa Ujerumani Stuttgart wamerudi tena kutamba pale jumamosi walipowazaba viongozi wa Ligi Bayern Munich mabap 3:1.

Mabingwa Stuttgart watamba upya ?

Mabingwa Stuttgart watamba upya ?

Katika Bundesliga,mabingwa watetezi Stuttgart wawachezesha viongozi wa Ligi Bayern Munich kindumbwe-nduimbwe waliopowacharaza mabao 3:1.

Katika Serie A-Ligi ya Itali polisi yampiga risasi shabiki wa Lazio Roma na kumua na hii yapalilia fujo .

Robinho atia mabao 2 katika ushindi wa mabao 4-3 wa Real Madrid dhidi ya Mallorca katika La Liga-Ligi ya Spian na China imeanzisha shirika la kupambana na madhambi ya doping kabla ya Olimpik.

Tutawachukua pia katika dimba nchini Tanzania,Kenya na Burundi.

Tuanze basi na ligi mashuhuri barani Ulaya:

Serie A, Ligi ya Itali imerudi tena kugonga vichwa vya habari baada ya polisi jana kumfyatulia risasi na kumuua shabiki wa Lazio Roma, wakati wakijaribu kuzima machafuko kati ya mashabiki wa lazio na wa Juventus huko Tuscany.Lazio ilikua ichezea na Inter Milan.

Masaa baadae mjini Roma, mashabiki wa Lazio wakazusha machafuko na kuhujumu kituo cha polisi karibu sana na Satdio Olimpico-olimpic stadium.Mamia ya chipukizi waliburura vizuwizi vya chuma kulizinga daraja la kupita karibu na uwanja huo w dimba.

Waliwasha pia moto na kuvunja dirisha la kituo cha polisi.Uwanja wa Olimpico ulikuwa mtupu baada ya polisi kuamua kuvunja mechi iliokuwa ichezwe usiku wa jana kati ya AS Roma na cagliari.Wakuu wa usalama walihofia kifo cha shabiki wa Lazio Roma huko Tuscany, kingezidisha ghadhabu za mashabiki uwanjani.

Kwa jumla mechi 3 zilivunjwa siku hiyo

Lakini mechi nyengine ziliendelea huku mabingwa Inter wakiendelea kuongoza baada ya Fiorentina kushindwa kwa mabao 2-1 na Udinese-üigo lao la kwanza katika jumla ya mechi 21 tangu April.

Ama katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani,rekodi ya mechi 24 bila kushindwa ya Bayern münich,imevunjwa na mabingwa watetezi VFB stuttgart .Munich ilichezesheshwa kweli kindumbwe-ndumbwe hapo jumamosi na mwishowe ikazabwa mabao 3:1.

Kocha wa B.Munich Ottmar Hitzfeld alilieleza hivi pigo hilo kali:

„Tulipwaya sana na tukishindwa changamoto za mtu na mtu jambo ambalo halieleweki ilikuaje.Tujkawa na shida ya kucheza mchezo wetu na ukicheza ngambo huwa huna tena nafasi ya kushinda na hasa baada ya adui kuongoza kwa mabao 2:0.“

Nae kocha wa mabingwa watetezi –Stuttgart, Armin

Veh alisema:

„Kwa jumla tumechezavizurikabisa kipindi cha kwanza.Nyuma tulijiandaa barabara na tulitia fora usoni.Tulitia bao wakati barabara.“

Kwa ushindi wa mabao 3:1 wa mabingwa Stuttgart, mwanya wa Bayern Munich kileleni ulipungua hadi pointi 1 huku Werder Bremen wakiwaandama .Bremen iliikomea Karlsruhe iliopo nafasi ya 4 kwa mabao 4-0 wakati hamburg iliacha nafasi ya kuparamia kileleni kwa mudu suluhu tu bao 1:1 na schalke 04.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza,Manchester United imefungua mwanya wa pointi 3 kati yake na Arsenal.Hii yafuatia ushindi wao wa mabao 2:0 dhidi ya Blackburn Rovers.Alikua Christiano Ronaldo alielifumania mara 2 lango la Blackburn.

Katika la Liga huko Spain, Real madrid imeseleleza mwanya wake wa uongozi wa pointi1 kufuatia ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Real Mallorca.Stadi wa Brazil Robinho alitia mabao 2 pekee na kupasia Raul kwa bao la 3.Barcelona inaendelea kupepesuka ,kwani ilizabwa mabao 2 na Gatafe.

Huko Holland Ajax Amsterdam imebakia kileleni mwa Ligi ya Holland kufuatia sare ya jana ya mabao 2-2 na hasimu wao Feynoord.Eindhoven wamezimwa sare 1-1 na Alkmaar.

Mwishoe, Olimpik Beijing 2008:

Chna imeamua kuanzisha shirika la kupambana na madhambi ya doping-matumizi ya madawa kuongeza kasi .Taasisi hiyo itakuwa karibu na uwanja wa olimpik na azma ya China ni kuhakikisha michezo ijayo ya olimpik itakuwa safi bila ya madhambi ya doping.

 • Tarehe 12.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHas
 • Tarehe 12.11.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHas