1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STRASSBURG: Vikosi vya Ulaya kulinda kambi za wakimbizi

28 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBM5

Bunge la Umoja wa Ulaya linaunga mkono kupeleka vikosi vya amani vya Ulaya nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati,kulinda kambi za wakimbizi katika nchi hizo mbili.Masharti ni kuwa vikosi hivyo visielemee upande wo wote na iwepo ratiba ya kuondoka.Lengo kuu la ujumbe huo ni kuleta utulivu katika eneo linalopakana na jimbo la mgogoro la Darfur,magharibi ya Sudan.