1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Srebrenica-bunge la Serbia labeba dhamana

Oumilkher Hamidou1 Aprili 2010

Serbia yakiri kuhusika na mauwaji ya wabosniak yaliyotokea miaka 15 iliyopita huko Srebrenica

https://p.dw.com/p/MjwW
Bibi huyo anaomboleza katika kiunga cha makaburi ya zaidi ya wabosniac elfu nane waliouliwa Srebrenica July mwaka 1995Picha: picture-alliance/ dpa

Bunge la Serbia mjini Belgrade lajibebesha dhamana ya kuuliwa wabosniak wa Srebrenica,idadi ya wasiokua na ajira yaanza kupungua nchini Ujerumani ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanzie basi katika eneo la Balkan ambako gazeti la "Münchner Merkur linajiuliza kama uamuzi wa bunge la Serbia mjini Belgrade haukushawishiwa kisiasa.

Gazeti linaendelea kuandika:

Serbia inataka kujiunga na Umoja wa ulaya.Na njia ya kuelekea Bruxelles ni ndefu.Lakini hata njia ndefu ina mwanzo wake.Belgrade imeianza njia hiyo kwa kuomba radhi kwa mauwaji ya Srebrenica.Lakini hatua hiyo ina maana gani?Ni ya dhati? Na maneno yatafuatwa kivitendo?"

Gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linaandika

"Bunge la Serbia limepitisha azimio kuhusu Srebrenica kwa shingo upande.Pekee matokeo ya nusu bin nusu ya kura iliyopigwa yanabainisha mgawanyiko uliopo katika jamii ya Serbia,miaka 15 baada ya mauwaji makubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa barani Ulaya baada ya mwaka 1945-na jinsi jamii inavyokabwa na shida ya kuishughulikia historia yake ya hivi karibuni.Hata hivyo ni jambo la kutia moyo kwamba bunge la mjini Belgrade limejibebesha jukumu la yaliyotokea.Hiyo ni hatua ya mwanzo kuelekea mustakbal mwema wa nchi hiyo.Pengine tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kumalizika,muda uliopita si mrefu hivyo kuweza kusahau machungu ya zamani.Hata muungano wa Ulaya ulihitaji muda baada ya mwaka 1945.Na waturuki mpaka leo bado hawajakiri kushiriki kwao katika mauwaji ya halaiki yaliyotokea miaka 100 iliyopita.

Mada ya pili magazetini inahusu tarakimu zilizotangazwa jana za kupungua idadi ya wasiokua na ajira nchini Ujerumani.Gazeti la "Der neue Tag" linaandika:

"Opereshini imefana,mgonjwa hajafa.Kwa ufupi,huo ndio ufafanuzi wa soko la ajira la Ujerumani.Lakini ishara ya kutia moyo iliyotolewa jana na taasisi kuu ya ajira nchini Ujerumani,haimaanishi kama soko la ajira ni imara.Kwasababu marekebisho ya takwimu ndiyo yaliyopelekea idadi ya wasiokua na kazi kuwa ndogo kuliko namna ilivyo.

Na gazeti la "Mitteldeutsche Zeitung" linaandika:

Si miujiza hata kidogo,ni matokeo ya sera za soko la ajira na jinsi hali ya wananchi namna ilivyo.Kombe hapo linalowasaidia wajerumani kutoka katika mgogoro ni ajira ya muda mfupi.Ingawa mkakati huo unagharimu fedha nyingi lakini angalao wafanyakazi wanaendelea kuwepo kazini.Zaidi ya hayo makampuni mengine yanawalipa fidia watumishi wake ili wakubali kustaafu kabla ya wakati .Mkakati huo lakini tija yake ni ya muda mfupi.Uchumi ukikua kweli mnamo msimu huu wa mapambazuko,hapo mkakati wa serikali wa kudhamini nafasi za kazi utaweza kusifiwa kua ni ufanisi.

Mawandishi:Hamidou,Oummilkheir/Dt Agenturen

Mpitiaji:Mohamed Abdul-Rahman