1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Somalia yasema imewaua wapiganaji 40 wa Al Shaabab

10 Julai 2023

Jeshi la Somalia limesema kwamba limewauwa karibu makamanda na wapiganaji 40 wa kundi la itikadi kali la Al-Shabaab ambalo linaongoza uasi dhidi ya serikali kuu mjini Mogadishu kwa miaka mingi.

https://p.dw.com/p/4Tgkz
Somalia Mogadishu
Vikosi vya usalama huko SomaliaPicha: Hassan Ali ElmiAFP/ Getty Images

Kamandi ya Jeshi la Marekani barani Afrika, AFRICOM, imesema ililisaidia jeshi la Somalia kufanya mashambulizi matatu ya anga wakati wa mapigano kusini mwa nchi hiyo karibu na mpaka na Kenya.

Kulingana na AFRICOM, wapiganaji 10 wa Al-Shabaab ndiyo wameuawa na hakuna kifo chochote cha raia. Marekani imekuwa ikiiunga mkono Somalia kwenye mapambao yake dhidi ya kundi hilo kwa kufanya mashambulizi ya kutumia ndege zisizo na rubani na msaada mwengine wa kiufundi.Al-Shabaab yadai kuhusika na shambulio kwenye hoteli mjini Mogadishu

Taifa hilo la Pembe ya Afrika lenye wakaazi wapatao milioni 16 limekuwa likiandamwa na mashambulizi ya Al-Shabaab na matukio mengine ya uhalifu wa kundi hilo kwa zaidi ya miaka 15.

Katika miezi ya  karibuni, serikali mjini Mogadishu imefanikiwa kusonga mbele kwa kuzilenga ngome za wapiganaji wa kundi hilo kupitia kampeni kubwa ya kijeshi.