1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia: Wanajeshi wa Kenya wakabiliana na wanamgambo wa Al Shabaab

14 Desemba 2011

Vikosi vya wanajeshi wa Kenya pamoja na wale wa serikali ya mpito ya Somalia wanaokabiliana na wanamgambo wa kiislam wa Alshabaab wanapanga kuingia ndani zaidi hadi katika maeneo yanayothibitiwa na waasi nchini humo.

https://p.dw.com/p/13ShN
Kenyan military board a truck headed to Somalia, near Liboi at the border with Somalia in Kenya, Tuesday, Oct. 18, 2011. Kenya said its launch of military operations into southern Somalia against al-Shabab militants was in response to the kidnappings of four Europeans over the last six weeks, though military analysts suspect that Kenya had prepared the invasion before the abductions. (Foto:AP/dapd)
Jeshi la Kenya nchini SomaliaPicha: dapd

Hayo yanajiri huku Umoja wa mataifa ukisema shilingi bilioni 1.5 zinahitajika ili kuyaokoa maisha ya Wasomali.

Miezi miwili baada ya serikali ya Kenya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia kukabiliana na wanamgambo wa Al shabaab walio na mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda, wanajeshi hao hawajakuwa na ufanisi mkubwa katika kutekeleza jukumu hilo kutokana na hali mbaya ya hali ya hewa huku nao wanamgambo hao wakizidisha mashambulizi ya grunedi na mabomu ya kutegwa ardhini katika maeneo yaliyo karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.

Msemaji wa kikosi cha jeshi la Kenya Cyrus Oguna anasema wamekuwa na changamoto chungu nzima katika harakati zao na wala sio hali mbaya ya hewa pekee iliyowatatiza.

Akizungumza katika eneo la kusini mwa Somalia la Ras Kamboni, Afisa wa Jeshi la Kenya Kapteni Thomas Mwanga amesema vikosi vyao bado vinalenga kuingia katika eneo la Kismayo.

FILE - This Dec. 8, 2008 file photo shows armed fighters from Somalia's al-Shabab jihadist movement traveling on the back of pickup trucks outside Mogadishu. Training camps in the lawless nation of Somalia are attracting hundreds of foreigners, including Americans, and Somalis recruited by a local insurgent group linked to al-Qaida, according to local and U.S. officials. American officials and private analysts say the camps pose a security threat far beyond the borders of Somalia, including to the U.S. homeland. (AP Photo/Farah Abdi Warsameh, File)
Wanamgambo wa AlShabab,MogadishuPicha: AP

Hata hivyo waziri wa ulinzi wa Kenya Yusuf Haji alisema mwezi huu kuwa lengo lao hasa sio Kismayo, ambalo ni mji muhimu wa bandari unaothibitiwa na wanamgambo wa Alshabaab. Naye Kapteni Mwanga amefafanua kuwa waziri alimaanisha kuwa jeshi la Kenya halitaumiliki mji wa Kismayo, bali watawafurusha tu wapiganaji na kuurejesha kwa uthibiti wa serikali ya mpito ya Somalia.

Msemaji wa serikali ya Somalia Mohamed Ibrahim Faraha amesema wanajeshi hao wanatahmini jinsi hali iliyo baada ya mvua kupungua katika eneo hilo katika siku za hivi karibuni. Amesema sasa watalazimika kusubiri siku zingine kumi kabla ya kufanya tena uamuzi mwingine.

Wanajeshi wa Kenya wako katika maeneo matatu kusini mwa Somalia. Makabiliano hayo yalizinduliwa katikati ya mwezi Oktoba baada ya msururu wa matukio ya utekaji nyara katika maeneo ya mipakani na mashambulizi ambayo serikali ya Kenya ililinyooshea kidole kundi la Alshabaab.

FILE - In this Tuesday, Aug. 24, 2010 file photo, Kenya Army soldiers rehearse a military parade at Uhuru Park, in Nairobi, Kenya. Kenyan military forces moved into southern Somalia on Sunday, an official and residents said, a day after top Kenyan defence officials said the country has the right to defend itself after a rash of militant kidnappings of Europeans inside Kenya. (Foto:Sayyid Azim, File/AP/dapd)
Wanajeshi wa KenyaPicha: dapd

Lakini mashirika ya misaada yanasuasua kuhudumu katika maeneo yanayothibitiwa na vikosi vya Kenya kwa sababu yanahofia mashambulizi zaidi. Kule Nairobi mjumbe wa maswala ya kiutu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Mark Bowden amesema wanahitaji shilingi bilioni 1.5 ili kufadhili mamia ya miradi ya kuokoa maisha, ikiwemo chakula, afya na elimu. Anasema hawawezi mzozo wa Somalia ni jukumu la kila mtu na kwamba Wasomali wanahitaji msaada sasa.

Wapiganaji wa kiislamu wanaothibiti maeneo mengi ya kusini na kati mwa nchi hiyo mwezi jana waliyazuia mashirika 16 ya kutoa misaada dhidi ya kuhudumu katika maeneo yaliyo chini ya uthibiti wao.

Ripoti: AFP

Mwandishi: Bruce Amani

Mhariri: Abdul-Rahman