Somalia: Baada ya miongo miwili ndege ya kimataifa yatua Mogadishu
6 Machi 2012Matangazo
Naibu waziri mkuu wa Uturuki aliyekuwa mmoja wa abiria katika ndege hiyo Bekir Bosdag amesema nchi yake imeanzisha rasmi shughuli za shirika hilo la ndege nchini Somalia.Hali ya usalama iliimarishwa katika uwanja huo wa ndege mapema leo asubuhi kabla ya kutua ndege hiyo iliyotokea Ankara.
Saumu Mwasimba amezungumza moja kwa moja kutoka Mogadishu na mbunge Hussein Bantu ambaye pia alikuweko kuwalaki wageni kutoka Uturuki na kwanza amezungumzia hisia zake juu ya kuwasili kwa ndege hiyo.
(Kusikiliza mazungumzo hayo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi : Saumu Mwasimba
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman