SOFIA: Maelfu waandamana Bulgaria wakitaka raia wao kuachiliwa nchini Libya. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SOFIA: Maelfu waandamana Bulgaria wakitaka raia wao kuachiliwa nchini Libya.

Kiasi watu elfu ishirini wameandamana mjini Sofia, Bulgaria wakitaka wauguzi watano raia wa nchi hiyo pamoja na daktari mmoja mpalestina waachiwe huru nchini Libya.

Watu hao wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa mashtaka ya kuwaambukiza virusi vya Ukimwi kwa maksudi watoto zaidi ya mia nne kwenye hospitali moja mjini Benghazi, Libya.

Maandamano hayo yanaadhimisha mwaka wa nane tangu watu hao wanne walipokamatwa.

Wataalamu wa afya wa kimataifa wamesema wauguzi hao hawakuhusika moja kwa moja ila hali mbovu ya usafi wa hospitali hiyo ndiyo iliyosababisha maambukizi hayo.

Kundi la mawakili wa Bulgaria linatarajia kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwenye Mahakama Kuu ya Libya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com