1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Sudan inahitaji mazungumzo ili kuvimaliza vita

Lilian Mtono
16 Agosti 2023

Naibu mkuu wa Baraza tawala nchini Sudan Malik Agar amesema kuna ulazima wa kuwa na serikali ya mpito nchini Sudan, kutokana na hali inayoshuhudiwa hivi sasa.

https://p.dw.com/p/4VDsV
Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akizungumza na wanajeshi wake
Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akizungumza na wanajeshi wakePicha: Sudanese Armed Forces/REUTERS

Malik Agar amesema hayo katika hotuba yake ya moja kwa moja kupitia televisheni na kuongeza kuwa mikakati ya kila wakati ya amani haina tija kwa taifa hilo na kuongeza kuwa njia pekee ya kumaliza mapigano, ni mazungumzo.

Mapigano nchini Sudan yanahusisha vikosi vya Sudan vinavyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na kikosi cha Dharura, RSF kinachoongozwa na Jenerali Hamdan Dagalo.

Watu zaidi ya milioni moja wamekimbilia nchi jirani na wengine milioni 3 na zaidi wakiyakimbia makazi yao, hii ikiwa ni kulingana na shirika la kimataifa la wahamiaji, IOM.