SIPRI na tathmini ya machafuko arabuni | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.06.2012
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

SIPRI na tathmini ya machafuko arabuni

Shirika la Utafiti wa amani la kimataifa International Peace Research Insitute (SIPRI) lenye makao yake mjini Stockholm Sweden leo limetowa matokeo ya utafiti wa mwaka 2012 unaotathmini hali ya usalama wa kimataifa.

Silaha

Silaha

Miongoni mwa mambo mengine, utafiti huo unaonyesha kuwa migogoro iliyojitokeza katika Kanda ya mashariki ya Kati imeonyesha wazi wazi mwenendo unaobadilika wa migogoro ya kivita.

Ripoti ya SIPRI ya mwaka 2012 inaonesha namna jamii ya kimataifa ilivyoshughulikia migogoro iliyoibuka katika kanda ya mashariki ya kati na Afrika kaskazini, ikiwa ni pamoja na operesheni iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa na kuendeshwa na vikosi vya Jumuiya ya Kujihami NATO nchini Libya, maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vikwazo na uzuiaji wa usafirishaji wa silaha, na ujumbe wa kwanza wa amani wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu kwenda nchini Syria.

Kufanana na tofauti za migogoro hii
Yakijumulishwa pamoja, matukio ya migogoro katika mataifa ya kiarabu yanaonyesha kuongezeka kwa mchangamano wa migogoro ya kivita. Wakati machafuko haya yalikuwa na mambo kadha yanayofanana - ikiwa ni pamoja na mandamano makubwa ya amani, kutokuwa na kiongozi mmoja wa mandamano, na matumizi ya viwanja vikubwa katika miji mikuu - lakini pia yalikuwa na tofauti kadhaa. Madai ya wanadamanaji yalitofuatiana, kuanzia kwenye hali bora ya uchumi hadi kwenye mabadiliko ya utawala.

Ripoti hii inasema matukio ya mwaka uliyopita hayakutofautiana sana katika mwelelekeo na migogoro iliyoendelea kujitokeza katika mataifa mbalimbali. Yalirudia mabadiliko yaliyokuwa yakitokea katika migogoro ya kivita kwa miongo kadhaa. Yakiwekwa pamoja, mabadiliko haya yanaonyesha kuwa kuna mazingira mapya ya migogoro yanayojitokeza, ambapo uingiliaji wa jumuiya ya kimataifa unakuwa mgumu kufanyika, anasema Dk. Neil Melvin, Mkurugenzi wa Programu ya Migogoro ya kivita ya SIPRI.

Nyambizi ya kivita.

Nyambizi ya kivita.

Kupungua kwa silaha za nyuklia
Ripoti hii inaonseha kupungua kwa silaha za nyuklia kati ya mwaka 2011 na 2012. Inasema mwanzoni mwa mwaka 2012, mataifa nane - Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa, China, India, Pakistan na Israel walikuwa na silaha za nyuklia zinazofanya kazi 4400 na karibu 2000 kati ya hizi zinawekwa katika hali ya tahadhari. Inasema kama vichwa vya silaha hizi vinahesabiwa, mataifa haya yote yana jumla ya silaha 19,000 ikilinganishwa na 20,530 mwanzoni mwa mwaka 2011.

Inasema upungufu huu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na juhudi za Marekani na Urusi kupunguza hazina yao ya silaha za nyuklia chini ya masharti ya Mkataba wa kupunguza sila za nyuklia uitwao Treaty on Measures for Further Reduction and Limitation of Strategic Offensive Arms (New START) na vile kupumzishwa kwa silaha zilizopitwa na wakati.

Operesheni za kulinda amani
Kwa mujibu wa ripoti hii machafuko haya pia yameonyesha kustawi kwa idadi ya walinda amani duniani kote, kukiwa na jumla ya watu 262,129 mwaka 2011 ikiwa ni pungufu ya watu 700 ikilinganishwa na mwaka 2010.

Bajeti ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2012 -2013 inatarajiwa kupungua, jambo ambalo linaweza kuathiri operesheni zinazoendelea za kulinda amani hivi sasa na uwezo wa Umoja huo kuendesha misheni nyingine na pia kupungua kwa shughuli za Umoja wa Mataifa huko mbeleni, anasema Mtafiti Mwandamizi, Sharon Wiharta, Mkuu wa Mradi wa Operesheni za amani wa SIPRI.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Mohammed Abdul Rahman.

 • Tarehe 04.06.2012
 • Mwandishi Admin.WagnerD
 • Maneno muhimu SIPRI, 2012, Report
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/157Y3
 • Tarehe 04.06.2012
 • Mwandishi Admin.WagnerD
 • Maneno muhimu SIPRI, 2012, Report
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/157Y3

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com