1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SINGAPORE: Bush amewasili Singapore akiwa ziarani bara la Asia

16 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsK

Rais George W.Bush amewasili Singapore,kituo cha kwanza cha ziara yake ya juma moja barani Asia,kupigia debe mageuzi ya kidemokrasi na kuimarisha uhusiano wa usalama na biashara kati ya Marekani na kanda hiyo.Ziara hii itampeleke pia Indonesia na Vietnam ambako siku ya Jumapili atahudhuria mkutano wa kilele utakaojadili masuala ya uchumi wa maeneo ya Asia na Pacifik-APEC.Kabla ya kuelekea nchi za Asia,rais Bush alitua Moscow ambako alikutana na rais wa Urussi Vladimir Putin.