1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Siku ya kupiga vita ubaguzi duniani

Ramadhan Ali21 Machi 2007

Ubaguzi umekua ikitia kichwa chake hata katika mchezo wa mpira.kabumbu likiongoza katika utandawazi huku wachezaji wa mataifa mbali mbali wakivuna fedha na kuwatumbuiza mashabiki nje ya mipaka ya nchi zao na mabara yao,umeanguka pia mateka ya wabaguzi viwanjani.

https://p.dw.com/p/CHHp
Biramu la Ujerumani la wiki dhidi ya ubaguzi
Biramu la Ujerumani la wiki dhidi ya ubaguzi

Katika miaka ya karibuni,mchezo wa mpira au kabumu ukichangia mno katika mfumo wa utandawazi umejionea pia visa vya ubaguzi hasa kwa wachezaji weusi ama kutoka Afrika au Brazil.

Visa vya ubaguizi katika viwanja vya dimba hasa Ulaya vimeripotiwa Itali,Uingereza,Ujerumani na karibuni vilitia fora nchini Spain.Wachezaji wengi maarufu wamekuwa usoni kuongoza vita hivi dhidi ya ukabila katika viwanja vya dimba-miongoni mwao mfaransa Thierry Henry anaeichezea Arsenal London na mkameroun Samuel Eto’o anaeichezea FC Barcelona.

Ujerumani wachezaji wa kiafrika na hasa Mashariki mwa Ujerumani wamekuwa mateka wa chuki za kikabila miongoni mwa baadhi ya mashabiki.Kuna wengine wakitupiwa ndizi viwanjani kuashiria wao ni nyani na warudi msituni.

Shirikisho la dimba la Ujerumani-DFB sawa na FIFA-shirikisho la kabumbu ulimwenguni, hata kabla ya kombe la dunia mwaka jana hapa Ujerumani, yalipania kupiga vita ukabila viwanjani.”Die welt zu gast bei Freunde”-walimwengu wanakaribishwa na marafiki zao-ndio upatu uliopigwa na kuhanikizwa na shirikisho la Ujerumani wakati wa kombe la dunia kuondosha dhana zozozte za ubaguzi na wajerumani wakatu nukiwa Kombe la dunia kuwa ndio waliokuwa mashabiki bora kati ya wote.

Hii haina maana kwamba visa vya bughdha za ukabila zimeondoka na Kombe la dunia,la hasha.

Wakati wa mpambano wa Bundesliga-Ligi ya Ujerumani kati ya Leverkusen na Borussia Mönchengladbach wiki 2 zilizopita –huku timu zote 2 zikiwa na wachezaji weusi ama kutoka Brazil au Afrika-muandishi wa Deutsche Welle- Josefa Martens alikwenda kupeleleza chuki zinavyozuka alipochanganyika na mashabiki uwanjani.Shabiki wa Bayer Leverkusen alimwambia:

“Binafsi nimecheza dimba kwa miaka 20 na nimecheza pia na wachezaji wengi raia wa kigeni.Kati yao kuna pia watu wazuri.Kuna wengi bora hata kupita baadhi ya wajerumani.”

Asema shabiki huyo wa kijerumani.

Kwanini ubaguzi unaingia viwanjani shabiki huyu wa Bayer Leverkusen inayocheza na Mbrazil, Juan, hajui ni kwanini.Anaongeza lakini:

“Naweza lakini kufikiria vipi inakuwa.Hujionea katika TV visa vinavyotokea hata huko mashariki mwa Ujerumani.

Katika uwanja wetu huu wa Leverkusen si sana kujionea visa kama hivyo.Ubaguzi pia unapita katika Ligi za daraja za chini kabisa yaani zile za mikoa na wilaya .Huko nisingependa kucheza dimba,kwani huko ningeingiwa na hofu.”

Prof.Walter Tokarski,mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha michezo mjini Cologne,amejionea tangu miaka mingi sasa fujo na uhuni unaozidi katika viwanja vya dimba.Anasemema:

“Hivi sasa vikundi vya mashabiki wa mpira vimevaa njuga kuzusha machafuko zaidi viwanjani na hasa vile vinavyojiita “Ultras’. Vikundi hivi vya Ultras sio tu vipo nchini Itali bali hata Ujerumani.

Vina siasa kali na hata kujitambulisha na vile vya mrengo wa kulia .Wakati wa mashindano ya mpira huja na mabiramu yao.Na hilo ndilo tatizo tulilonalo hii leo.Kwani, hawabakii na mabiramu yao tu bali huzusha fujo na vita viwanjani.”

Shirikisho la michezo la vijana la Ujerumani-“Dt.Sportjugend” kwahivyo, limeitisha wiki ya kupiga vita ubaguzi .

Majadiliano wazi wazi na kuchukua msimamo wazi dhidi ya ukabila bado hayapo tangu kutoka viongozi wa mashirika ya spoti hata wachezaji na hata kati ya mashabiki viwanjani.Alao Shirikisho la dimba la Ujerumani-DFB na FIFA- yameshaamka kuzuwia ubaguzi na chuki katika mchezo maarufu na unaowatia wake kwa waume, wakubwa kwa wadogo wazimu-mchezo wa mpira.