Shirika la Ndege la Zimbabwe lanyang′anywa ndege | Matukio ya Afrika | DW | 18.05.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Shirika la Ndege la Zimbabwe lanyang'anywa ndege

Shirika la Ndege la Zimbabwe limefuta safari zake zote za ndege katika eneo la Afrika, baada ya kupokonywa ndege moja ya kodi kwa sababu ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya dola 460,000 za Kimarekani.

Rais Robert Mugabe (kushoto) na Waziri Mkuu wake, Morgan Tsavingirai

Rais Robert Mugabe (kushoto) na Waziri Mkuu wake, Morgan Tsavingirai

Kwa mujibu wa mkuu wa shirika hilo la Air Zimbabwe, Innocent Mavhunga, hatua hiyo imelifanya shirika lake kubakia na safari moja tu ya kutoka Harare kuelekea London, pamoja na safari nyingine mbili za ndani ya nchi.

Air Zimbabwe ilikuwa imekodi ndege aina ya Boeing 737-500 kutoka shirika moja la ndege la Zambia linaloitwa Zambezi, lakini sasa Zambezi limeichukua ndege yake.

Mgogoro huo umekuja siku chache baada ya shirika hilo la ndege la Zimbabwe kutimuliwa kutoka chama kinachohusika na safari za ndege za Kimataifa, IATA, kutokana na kudaiwa zaidi ya dola 280,000 za Kimarekani.

Mwandishi: Saumu Ramadhani Yusuf
Mhariri: Mohammed Khelef

 • Tarehe 18.05.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11IzM
 • Tarehe 18.05.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11IzM